Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:25

Wanamgambo wenye msimamo mkali wadai kuhusika na shambulizi la DRC


Wanamgambo wenye msimamo mkali Jumatatu wamedai kuhusika na shambulizi la kanisani mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika shambulizi hilo serekali imesema idadi vifo vya shambulizi hilo la Jumapili vimefikia 14.

Kundi la Islamic State na chombo chake cha habari cha Aamaq kimetoa taarifa ikisema kwamba wanamgambo walitega mlipuko ndani ya kanisa la Kipentakoste mjini Kasindi na kulipuka wakati watu wakiwa wanasali.

Taarifa ya kundi hilo imesema kwamba itakata kuona vikosi vya Congo vinafahamu kwamba mashambulizi yao yataendelea kwa utashi wa kijihadi na yatavidhoofisha zaidi na kufanya vishindwe.

Wenye msimamo mkali wamedai bomu lao limeua wakristu 20.

Serekali ya Congo imesema waliokufa ni 14 na wengine 63 kujeruhiwa na walipelekwa katika hospitali ya serekali ya Goma na walinda amani wa tume ya Umoja wa Mataifa inayojulikana kama MONUSCO.

XS
SM
MD
LG