Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:08

Wanamgambo wauwa polisi wanne na kujeruhi wengine Pakistan


Shambulizi Pkistan
Shambulizi Pkistan

Shahid Hameed msemaji wa kituo cha polisi cha Lakki ameliambia gazeti la Dawn kwamba wanamgambo hao walivamia kituo majira ya usiku lakini hawakufanikiwa kuingia ndani ya jengo na walikimbia. Taarifa ya shirika la habari la Associated press imesema washambuliaji walitumia magruneti na silaha nyingine katika shambulizi lao.

Hata hivyo taarifa zinasema kwamba polisi inashutumu kundi la wanamgambo la Tehreek-i-taliban Pakistan, lililopigwa marufuku linaweza kuwa limehusika na shambulizi hilo. Maafisa wanasema hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo.

Mwezi uliopita wanamgambo walivamia msafara wa doria wa polisi unaofanyika kila wakati na kuwauwa polisi wote sita waliokuwemo ndani ya gari katika eneo la Dadewala katika wilaya ya Lakki Marwat.

Kundi la Taliban lilidai kuhusika na shambulizi hilo. Katika tukio jingine mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijilipua mwenyewe karibu na gari kubwa lililokuwa limebeba maafisa wa polisi wakiwa njiani kutoa ulinzi kwa wafanyakazi wa huduma ya chanjo ya Polio karibu na Quetta, kusinimagharibi mwa Pakistan mwezi uliopita, ambapo pia polisi mmoja aliuwawa na wanafamilia watatu waliokuwa wanasafiri na gari waliokuwa karibu na tukio pia walikufa.

Bomu hilo lilijeruhi pia watu wengine 23 wengi wakiwa polisi.

XS
SM
MD
LG