Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 07:04

Marekani "yashtushwa" na mauaji ya mwandishi Mmarekani


Mwandishi habari wa Marekani James Wright Foley.
Mwandishi habari wa Marekani James Wright Foley.

Wanamgambo wa Islamic State walitoa video inayodai kuthibitisha kuchinjwa kwa mwandishi James Wright Foley, ikisema ni ujumbe kwa Marekani kuacha kuingilia kati maswala ya Iraq.

Utawala wa rais Barack Obama unasema unajaribu kuthibitisha tukio kwenye ukanda wa video unaoonyesha mauaji ya mwandishi wa habari wa Marekani, James Wright Foley aliyeuawa na wanamgambo wa Islamic State (I.S.)

Jumanne kundi hilo la wanamgambo wa Islamic State lilitoa video inayodai kuthibitisha kukatwa kichwa kwa Bw. Foley, ikisema ni ujumbe kwa Marekani kuacha kuingilia kati maswala ya Iraq.

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Caitlin Hayden, alisema ikiwa habari hizo ni sahihi, Marekani inalaani mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari huyo asiye na hatia na kutuma rambi rambi za dhati kwa familia yake pamoja na marafiki.

Hayden alisema maafisa wa kijasusi wa marekani wanafanya kazi haraka kuchunguza ukweli wa madai kwenye video hiyo.

Foley alikuwa akiripoti matukio ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria alipotoweka Novemba mwaka wa 2012.

XS
SM
MD
LG