Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:51

Wanamgambo waanza kuondoka Tripoli


Waandamanaji wakiandamana kutoa wito kwa wanamgambo kuondoka mjini Tripoli, November 15, 2013
Waandamanaji wakiandamana kutoa wito kwa wanamgambo kuondoka mjini Tripoli, November 15, 2013
Wapiganaji wa jeshi la mgambo huko Libya wanaolaumiwa kwa ghasia mbaya mjini Tripoli tangu kuanguka kwa Moammar Ghadafi walianza kuondoka katika mji mkuu Jumatatu huku vikosi vya jeshi la Libya vikiingia kuhakikisha usalama mitaani.

Wanamgambo kutoka pwani ya mji wa Misrata walianza kuondoka kuelekea mashariki baada ya kutokea ufyatuaji risasi kwa waandamanaji Ijumaa na kuchochea siku mbili za mapambano ambayo yaliuwa watu wasiopungua 46 na kuwajeruhi mamia wengine.

Pia Jumatatu naibu mkuu wa upelelezi nchini Libya, Mustafa Nuh aliachiwa huru na watekaji nyara wake siku moja baada ya kumkamata wakati akiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.

Haikufahamika ni nani alimteka Nuh ambaye familia yake inatokea Misrata.
XS
SM
MD
LG