Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 21:03

Kamanda wa IS ajeruhiwa vibaya


Msichana wa Syria aliyekoseshwa makazi
Msichana wa Syria aliyekoseshwa makazi

Wanamgambo wa Islamic State walielezea kwamba kamanda wa kundi hilo alijeruhiwa vibaya lakini hakuuwawa katika shambulizi la anga la wiki iliyopita.

Kundi linalofuatilia ghasia nchini Syria linasema wanamgambo wa Islamic State walielezea kwamba kamanda wa kundi hilo alijeruhiwa vibaya lakini hakuuwawa katika shambulizi la anga la wiki iliyopita.

Kundi hilo lenye makazi yake Uingereza la “Syrian Obsevatory for Human Rights” limesema leo kwamba Tarkhan Batirashvili ambaye pia anajulikana kama Abu Omar al-Shishani ama “Omar Chenche” alichukuliwa baada ya shambulizi la anga kwenda kwenye ngome kuu ya Islamic State mjini Raqqa, nchini Syria kwa matibabu.

Maafisa wa Marekani wamesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa aliuwawa na shambulizi la anga karibu na mji wa kaskazini mashariki wa al-Shaddadi.

XS
SM
MD
LG