Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:47

Wanamgambo wa Alshabab wapata ujasiri katika mashambulizi yao

Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.

Wanamgambo wenye itikadi kali wa Al-Shabab nchini Somalia wanapata ujasiri katika mashambulizi yao na wameongezeka kwa kutumia washambuliaji wa kujitoa mhanga wanaovalia vilipuzi vya kutengenezwa  majumbani katika kile ambacho wataalam wa usalama wanakiita mabadiliko ya mbinu.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu liliendesha moja ya mashambulizi mabaya zaidi siku ya Jumatano, likilenga uchaguzi katika ikulu ya ya rais katika mji wa Beledweyne karibu kilomita 300 kaskazini mwa Mogadishu. Watu 48 waliuawa, na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Miongoni mwa waliofariki ni mbunge, Amina Mohamed, mkosoaji mkubwa wa serikali, ambaye alikuwa kwenye kampeni alipolengwa na kuuawa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyevalia fulana ya vilipuzi.

Saa chache kabla, wanamgambo wawili wa Shabab walivunja boma lililokuwa na ngome nyingi katika uwanja wa ndege wa Mogadishu, ambapo uchaguzi wa rais umepangwa kufanyika. Ofisi za Umoja wa Mataifa, balozi za Magharibi na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika ziko katika eneo moja.

XS
SM
MD
LG