Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:03

Al-Shabaab yavamia kambi ya jeshi la Kenya


Wanajeshi wa KDF, nchini Somalia
Wanajeshi wa KDF, nchini Somalia

Ripoti za hivi punde zinasema kuwa wanamgambo wa Al-Shabaab wamevamia kambi moja ya jeshi la Kenya katika mjiwa DHAMESE, eneo la Gedo, lililo Kusini Magharibi mwa Somalia.

Tovuti ya kibinafsi ya Shabelle Media Netwok nchini Somalia imeripoti kuwa mizinga iliyofyatuliwa ililenga kambi ya jeshi la Kenya na ilisababisha uharibifu ambao haujadhibitishwa.

Ripoti hiyo imesema kuwa wanajeshi wa Kenya pia walifyatua mizinga wakati wa makabiliano hayo.

Radio Shebelle imemnukuu shahidi aliyeshuhudia tukio hilo akisema kuwa ufyatuaji wa mizinga ambao ulifanywa na wanajeshi wa Kenya, pia ulisababisha hasara ambayo haijadhibitishwa. Kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na shambulio hilo.

Kumekuwa na hali ya taharuki baina ya majeshi ya Kenya na wanamgambo wa Alshabaab katika siku chache zilizopita.

XS
SM
MD
LG