Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:21

Jeshi la Kenya lashambulia Al-Shabaab Somalia


Somali soldiers help a colleague who is wounded by Al-Shabaab gunmen.
Somali soldiers help a colleague who is wounded by Al-Shabaab gunmen.

Wizara ya Ulinzi ya Kenya inaaeleza kwamba wanajeshi wake huko Somalia wamewauwa wanamgambo ishirini na mmoja wa Al-Shabaab.

Wanamgambo hao waliuawa siku ya Jumanne karibu na mji wa Hawina, katika jimbo la kusini la Lower Juba huko Somalia. Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanari David Obonyo, amesema kwamba waliouawa ni pamoja na kamanda wa ngazi ya chini, Salad Bart, ambaye aliaminika kuwa kiongozi wa kundi hilo.

Obonyo amesema wanajeshi wa Kenya walikuwa wakielekea Tabda kutoka Dobley, na walipokaribia Hawaina, mwanamgambo mmoja wa Al-Shabaab aliwafyatulia risasi na kutoroka.

Gazeti la 'Daily Nation' limemnukuu Kanari Obonyo akisema kuwa hakukuwa na maafa yoyote kwa upande wa wanajeshi wa Kenya.

Wizara ya Ulinzi imeeleza kuwa bunduki kumi na saba aina ya AK-47, na silaha zingine mchanganyiko zilipatikana katika eneo la tukio hilo.

XS
SM
MD
LG