Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:21

Wanamgambo 16 wa Mai Mai wauwawa na jeshi la DRC


Vifaru pamoja na wanajeshi wa jeshi la Congo.
Vifaru pamoja na wanajeshi wa jeshi la Congo.

Wanachama wapatao 16 wa kundi la wanamgambo wa Mai Mai wameuwawa katika jimbo tete la Kivu kaskazini huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC chanzo kimoja cha jeshi kilisema Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP kundi hilo la wanamgambo lilihusika katika mapigano makali dhidi ya jeshi la Congo tangu Ijumaa wakati wanamgambo wasiopungua wanne walipokufa.

Msemaji wa jeshi Jules Tshikudi aliiambia AFP kwamba wanajeshi wa Congo waliwauwa wanamgambo saba wengine siku ya Jumapili na miili ya wanamgambo watano wa Mai Mai kundi linalojitambulisha lenyewe kama la “utetezi” ilipatikana Jumatatu. Hali hivi sasa imedhibitiwa alisema Tshikudi.

Mapigano yanazidi mashariki mwa DRC.
Mapigano yanazidi mashariki mwa DRC.

Ghasia zilitokea katika kijiji cha Kipese huko Lubero mashariki mwa eneo la maziwa makuu karibu na mpaka na Uganda. Mkoa huo upo kiasi cha kilomita 270 kaskazini mwa Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini mahala ambako mapigano kati ya makundi ya wanamgambo na jeshi la Congo yameongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka.

Mai Mai kwanza walijitokeza kama makundi ya kutetea jamii yaliyoundwa katika misingi ya kikabila.

XS
SM
MD
LG