Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:09

Wanajeshi wawili wa Bahrain wauwawa mpakani mwa Yemen na Saudi Arabia


Wanajeshi wawili kutoka Bahrain waliuawa kwenye mpaka kati ya Yemen iliyokumbwa na vita na Saudi Arabia, jeshi la Bahrain limesema Jumatatu, katika shambulio lilionyesha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Wanajeshi hao waliuawa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kitaifa ya kulinda mipaka ya kusini ya ufalme Saudi Arabia, ambayo imeongoza muungano wa kijeshi dhidi ya waasi wa Houthi wa Yemen tangu 2015, jeshi lilisema katika taarifa.

Tukio hilo lilitokea wakati Saudi Arabia, ikishinikiza kusitishwa kwa mapigano kwa muda mrefu karibu mwaka mmoja na nusu baada ya kukubaliana na Wahouthi ambapo kwa kiasi kikubwa yamefanyika licha ya kumalizika rasmi Oktoba mwaka jana.

Taarifa ya jeshi la Bahrain imesema kitendo cha kigaidi kilifanywa na ndege zisizo na rubani za Houthi katika eneo lisilojulikana kusini mwa Saudi Arabia.

Forum

XS
SM
MD
LG