Maafisa hao wamefika kwenye kambi hiyo wakati waandamanaji wakizingira majengo ya ofisi za rais, saa chache kabla ya wakati waliokuwa wamepanga kuondoka. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, waandamanaji hao walikuwa wameahidi kuondoka eneo hilo baadaye Ijumaa, baada ya baraza jipya la mawaziri kutangazwa na rais mpya aliyeapishwa Ranil Wickremesinghe.
Walioshuhudia wanasema kwamba waliona wanajeshi wakizunguka ofisi hizo zilizopo karibu na bahari, wakati wakivunja vibanda vya muda, vilivyowekwa na maelfu ya waandamanaji tangu Aprili. Maafisa walitumia vyombo vya kupasa sauti kuomba watu waliokusanyika waondoke kwenye eneo hilo.
Waandamanaji wa kampeni ya GoHomeGota, waliokuwa wakishinikiza kuondoka kwa rais Gotabaya Rajapaksa, wamekuwa wakikita kambi kwenye makazi ya rais, kabla ya kumlazimisha kutoroka Julai 9. Baada yake kuondoka, Wickremesighe alishika usukani wakati huo akiwa waziri mkuu.