Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:26

Wanajeshi watatu wa Ufaransa wauwawa Libya


Wizara ya ulinzi ya Ufaransa imetangaza vifo vya wanajeshi wake watatu waliouwawa nchini Libya.

Wizara ya ulinzi ya Ufaransa imetangaza vifo vya wanajeshi wake watatu waliouwawa nchini Libya. Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian alisikitika kutangaza kupoteza wanajeshi watatu wa Ufaransa ambao walifariki dunia wakiwa kazini nchini Libya. Wizara hiyo ilitoa taarifa iliyoelezea kuwapongeza wanajeshi hao kwa ushujaa wao na kujitolea kwao katika jeshi la Ufaransa kama wafanyakazi wake ambao kila siku hufanya kazi ya hatari ya kupambana na magaidi. Wizara hiyo haikuelezea namna wanajeshi hao walivyo uwawa japokuwa taarifa ya wanajeshi hao inakuwa ya kwanza kuripoti kuuwawa kwa wanajeshi toka ilipojulikana mwanzoni mwa mwaka huu kwamba vikosi maalumu vilikuwa vikifanya oparesheni nchini Libya

Wizara hiyo ilitoa taarifa iliyoelezea kuwapongeza wanajeshi hao kwa ushujaa wao na kujitolea kwao katika jeshi la Ufaransa kama wafanyakazi wake ambao kila siku hufanya kazi ya hatari ya kupambana na magaidi.

Wizara hiyo haikuelezea namna wanajeshi hao walivyo uwawa japokuwa taarifa ya wanajeshi hao inakuwa ya kwanza kuripoti kuuwawa kwa wanajeshi toka ilipojulikana mwanzoni mwa mwaka huu kwamba vikosi maalumu vilikuwa vikifanya oparesheni nchini Libya

XS
SM
MD
LG