Maafisa wa Pakistan wamesema Jumamosi kuwa bomu la kujitoa mhanga la ndani ya gari na shambulizi la bunduki katika kambi ya jeshi kwenye eneo karibu na mpaka wa Afghanistan liliwaua wanajeshi wasiopungua saba, wakiwemo maafisa wawili, na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulizi hilo la mapema asubuhi lilitokea katika wilaya tete ya mpakani ya North Waziristan, ambako wanamgambo wenye uhusiano na kundi lililopigwa marufuku la Tehrik-e-Taliban Pakistan au TTP, mara kwa mara wanavilenga vikosi vya usalama.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani shambulizi hilo kuwa ni kitendo cha kihuni cha magaidi, ofisi yake imesema. Taarifa ya jeshi imesema kuwa kundi la wanamgambo sita, walipuaji wa kujitoa muhanga, walishambulia kambi hiyo katika mji wa Mir Ali.
Forum