Mashambulizi hayo ya anga yalilenga wanajeshi wa utawala wa Syria, na ngome za kijeshi na ghala za silaha zinazotumiwa na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Teheran, kulingana na taasisi ya the Syrian Observatory for Human Rights.
Kwa zaidi ya muongo mmoja wa vita nchini Syria, nchi jirani ya Israel ilifanya mamia ya mashambulizi ya anga kwenye ardhi ya Syria, ikilenga hasa wanajeshi wanaoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah, vile vile ngome za jeshi la Syria.
Rami Abdel Rahman, kiongozi wa taasisi hiyo inayofuatilia vita, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi wanne wa Syria akiwemo afisa mmoja, pia wapiganaji wawili wanaoungwa mkono na Iran waliuawa katika mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za makundi yanayoungwa mkono na Tehran na ghala za zana za kijeshi na silaha.
Ameongeza kuwa wanajeshi wawili wa utawala wa Syria na wapiganaji watano wa kigeni walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Forum