Erdogan ameliambia shirika la habari la Uturuki TRT kwamba kiongozi wa IS, anayejulikana kama Abu Hussein al-Quarayshi, aliuawa katika shambulizi lililofanyika Jumamosi.
Amesema kwamba maafisa wa ujasusi wa Uturuki wamekuwa wakifuatilia Abu Hussein al-Qurayshi kwa muda mrefu.
Amesema kwamba Uturuki itaendelea kuwasaka makundi ya kigaidi bila ubaguzi wowote.
Mwanajeshi wa Syria, ameliambia shirika la habari la AP kwamba makabiliano dhid ya wapiganaji wa IS yametokea katika Kijiji cha Miska, mkoa wa Aleppo, ijumaa usiku.
Al-Qurayshi anaripotiwa kujilipua, mapigano yalipoongezeka zaidi.