Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:23

Wanajeshi wa UN kutoka Tanzania wauawa DRC


Walinda amani wa vikosi vya Monusco nchini DRC
Walinda amani wa vikosi vya Monusco nchini DRC

Wanaoshukiwa kuwa ni waasi wamewauwaa siyo chini ya walinda amani 14 wa Umoja wa Mataifa (UN) na askari watano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shambulizi hilo lilitokea kwenye kambi ya UN upande wa Mashariki ya Congo Alhamisi usiku, Ofisi ya UN imesema Ijumaa.

Vyanzo vya habari vimemkariri Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akisema kati ya waliouawa, anagalau wanajeshi 12 ni kutoka Tanzania.

Rais John Magufuli Tanzania alitumia ujumbe wa twitter kutuma salamu za pole kwa jeshi la Tanzania na kusema amepokea habari za vifo vya wanajeshi hao kwa mshtuko mkubwa.

Katibu Mkuu Guterres pia amelaani vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wowote mwengine wa kivita.

Guterres ameitaka DRC kufanya uchunguzi juu ya shambulio hilo na waliohusika kuchukuliwa hatua.

Wakati huohuo walinzi wa amani 53 wa UN katika vikosi hivyo walijeruhiwa, taarifa ya UN imesema.

Ofisi ya UN inayojulikana kama Monusco huko DRC imesema kuwa inaratibu kujibu shambulizi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Congo.

Pia ofisi hiyo inafanya matayarisho ya kuwapatia matibabu wale waliojeruhiwa kutoka katika kituo hicho cha kijeshi upande wa eneo la Kaskazini mwa Beni.

XS
SM
MD
LG