Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:31

Wanajeshi wa Ukraine waonekana wakilipua daraja kuyazuia majeshi ya Russia


Baada ya shambulizi la kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lysychansk, mashariki ya Ukraine, May 9, 2022,. (Photo by Yasuyoshi CHIBA / AFP)
Baada ya shambulizi la kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lysychansk, mashariki ya Ukraine, May 9, 2022,. (Photo by Yasuyoshi CHIBA / AFP)

Picha ambazo hadi sasa AP haijaweza kuzithibitisha, zilionyesha wanajeshi walio na silaha na sare za kijeshi wakiunganisha vilipuzi kwenye daraja.

Baadae walikwenda katika eneo salama kabla ya kutegua. Picha hizo pia zimeonyesha picha ambazo zimechukuliwa na drone.

Kwa mujibu wa walinzi wa kitaifa wa Ukraine daraja hilo kuvuka mto Siversky Donets liko kati ya Rubizhne na Lysychansk.

Gavana wa kijeshi wa eneo hilo, Serhiy Hidai amesema Jumatatu kwamba vikosi maalumu vya Ukraine vililipua madaraja ya reli yanayoshikiliwa na Russia kati ya Rubizhene na Severodonetsk kama sehemu ya juhudi za kupunguza kasi ya mashambulizi ya Russia.

Hata hivyo vikosi vya Russia kwa wiki kadhaa vimejaribu kuukamata mji wa Severodonetsk , eneo muhimu katika Donbas ambalo liko nje ya kitongoji cha wanaotaka kujitenga wamelishikiliwa kwa miaka kadhaa sasa


XS
SM
MD
LG