Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 20:31

Msemaji wa jeshi la Uganda asimulia madhila yaliyowapata wanajeshi wao Somalia


Wanajeshi wa UPDF waliopelekwa Somalia. Picha na LUIS TATO / AFP.
Wanajeshi wa UPDF waliopelekwa Somalia. Picha na LUIS TATO / AFP.

Msemaji wa jeshi la Uganda, UPDF, ameiambia VOA kwamba wanajeshi wa Uganda walijificha kwa siku sita kabla ya kuokolewa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kuteka kambi yao.

Brigedia Jenerali Felix Kulaigye alisema wanajeshi hao wanne, akiwemo Luteni mmoja, walinusurika kwa kujificha ndani na kando ya kambi hiyo iliyoko katika mji wa Bulo Marer, kilomita 110 kusini mwa Mogadishu.

Alisema wanajeshi hao walipatikana baada ya wanajeshi wa Uganda kkukomboa kambi hiyo siku ya Alhamisi.

"Tulipowaokoa, walikuwa dhaifu kwa sababu walikuwa wakiishi kwa kunywa mkojo," alisema Kulaigye.

Alisema kila askari alikuwa amejificha peke yake, katika maeneo tofauti.

"Walikuwa dhaifu kutokana na njaa," alisema."Luteni alikuwa amejeruhiwa, mguu wake ulikuwa katika hali mbaya na wanapata matibabu katika hospitali, na wanamatumaini watapona haraka."

Habari hizi zimetolewa baada ya Rais Yoweri Museveni aliposema kuwa wanajeshi 54 wa Uganda waliuawa katika shambulio hilo lililotokea tarehe 26 mwezi Mei.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda akizunguma na waandishi wa shirika la habari la Reuters.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akizunguma na waandishi wa shirika la habari la Reuters.

Uganda ilituma timu inayoongozwa na kamanda wa jeshi la nchi kavu Luteni Jenerali Kayanja Muhanga kwenda Somalia kufanya uchuguzi wa shambulio hilo.

Museveni aliwataja makamanda wawili kuwa walifanya "kosa" la kuwaamuru wanajeshi wao kurudi nyuma.

"Wamekamatwa na watakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kijeshi," alisema Museveni.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab siku ya Jumatatu lilichapisha video inayoaminika ni ya shambulio hilo kwenye kambi ya UPDF. Katika video hiyo, kiongozi wa al-Shabab, Ahmed Umar Abu Ubaidah, ambaye uso wake ulikuwa umetiwa ukungu, alionekana akitoa amri kwa wapiganaji wake..

Forum

XS
SM
MD
LG