Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:42

Wanajeshi wa Sudan Kusini wamewashambulia waasi huko Malakal


Vifaru vya jeshi la Sudan Kusini vikiwa eneo la waasi nchini humo. July 16, 2016.
Vifaru vya jeshi la Sudan Kusini vikiwa eneo la waasi nchini humo. July 16, 2016.

Jeshi la Sudan Kusini linaeleza kwamba wanajeshi wake wamewaua zaidi ya waasi 50 na wafuasi wa kundi la wanamgambo na kuwajeruhi wengine kadhaa wakati wa mapambano ambayo yalifanyika jumapili, magharibi ya mji wa Malakal.

Msemaji wa jeshi, Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang akiongozana na kundi la waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kwenda kwenye tukio la mapigano katika jimbo la Upper Nile mahala ambako alisema wanajeshi wa serikali walisababisha majeraha makubwa kwa wapiganaji wanaomtii Makamu Rais wa kwanza wa zamani, Riek Machar.

Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar.
Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar.

Koang alisema zaidi ya waasi 56 waliuwawa na walikamata silaha mbali mbali zaidi ya 200 pamoja na kushambulia miji miwili ya Alelo na Warjwok ambayo mpaka hivi sasa bado yamebaki chini ya udhibiti wao.

Msemaji huyo wa jeshi aliendelea kusema kuwa idadi ya vifo kwa wanajeshi wa SPLA In Opposition inaweza kuongezeka. Alisema wapiganaji wa SPLA walipoteza wapiganaji wane na angalau 20 wengine walijeruhiwa katika mapambano ambayo yalianza Ijumaa jioni.

XS
SM
MD
LG