Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 18:32

Wanajeshi wa Somalia wameuwawa na kujeruhiwa


Baadhi ya wanajeshi wa Somalia mjini Mogadishu

Wanajeshi wapatao wanne wa serikali ya Somalia wameuwawa na sita wamejeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na mjitolea mhanga ambaye alishambulia mgahawa mmoja wa chai katika mji uliogawanyika wa Galkayo huko kati kati ya Somalia, mashahidi na maafisa walisema Jumamosi.

Shambulizi hilo lilitokea upande wa kaskazini mwa mji unaodhibitiwa na jimbo lenye mamlaka yake yenyewe la Puntiland. Shahidi mmoja aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba kijana mmoja aliyevalia koti la vilipuzi aliingia ndani ya mgahawa mahala ambako maafisa wa usalama wa serikali na walinzi wao walikusanyika na kisha alijilipua.

Ramani ya somalia
Ramani ya somalia

Maafisa wa serikali katika jimbo hilo wamethibitisha kwamba makamanda wawili waandamizi wa jeshi walikuwa miongoni mwa waliokufa katika shambulizi hilo. Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika kwa shambulizi hilo lakini lilionekana kuwa ni shambulizi lililofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab.

Kundi hilo limeshambulia darzeni ya majengo ya serikali, mahoteli, na malengo mengine huko Mogadishu katika miaka ya karibuni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG