Wanajeshi wa Mali na kundi la Wagner, wanashutumiwa pia kuharibu na kuiba mali za rai, pamoja na kuwatesa wafungwa waliokuwa wanazuiliwa katika kambi ya jeshi.
Shirika hilo la haki za kibinadamu limesema kwamba limehoji watu 40 wenye ufahamu kuhusu tukio hilo, wakiwemo watu 20 waliodhulumiwa, wanafamilia watatu wa watu walioathiriwa, viongozi wawili wa kijamii, wanaharakati watano, waakilishi wanane wa mashairika ya kimataifa, pamoja na wachambuzi wa siasa wawili katika eneo la Sahel.
Waziri wa mambo ya nje wa Mali Aodoulaye Diop ametoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuondoa wanajeshi wa amani wa umoja wa mataifa, nchini Mali – MINUSMA, haraka iwezekanavyo kutokana na ukosefu wa Imani kati ya maafisa katka serikali ya Mali na wanajeshi wa umoja wa mataifa nchini humo wapatao 15,000.
Forum