Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:10

Wanajeshi wa Marekani wapata majeraha katika juhudi za kutengeneza gati la muda kwenye pwani ya Gaza


Lori la kubeba misaada ya kibinadamu katika eneo la Trident Pier, gati ya muda ya kupeleka misaada, nje ya Ukanda wa Gaza,Mei 19, 2024. U.S.(REUTERS).
Lori la kubeba misaada ya kibinadamu katika eneo la Trident Pier, gati ya muda ya kupeleka misaada, nje ya Ukanda wa Gaza,Mei 19, 2024. U.S.(REUTERS).

Wanajeshi watatu wa Marekani walipata majeraha yasiyo ya kivita katika juhudi za kutengeneza gati la muda kwenye pwani ya Gaza ikiwa ni njia ya misaada ya kibinadamu, huku mmoja akiwa katika hali mbaya

Wanajeshi watatu wa Marekani walipata majeraha yasiyo ya kivita katika juhudi za kutengeneza gati la muda kwenye pwani ya Gaza ikiwa ni njia ya misaada ya kibinadamu, huku mmoja akiwa katika hali mbaya kwenye hospitali ya Israel, maafisa wa Marekani walisema Alhamisi.

Majeraha hayo yalikuwa ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani wakati wa operesheni ya hivi karibuni ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina

Gati hilo lilitangazwa na Rais wa Marekani Joe Biden mwezi Machi na kuhusisha jeshi kujenga muundo unaoelea pwani.

Inakadiriwa kugharimu dola milioni 320 kwa siku 90 za kwanza na kuhusisha takriban wanajeshi 1,000 wa huduma wa Marekani, ilianza kufanya kazi wiki iliyopita.

Makamu Admirali wa Marekani Brad Cooper, naibu kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wawili kati ya wanajeshi hao walikuwa na majeraha ya kifundo cha mguu na majeraha madogo ya mgongo.

Forum

XS
SM
MD
LG