Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:16

Wanajeshi wa Marekani walioamriwa kuondoka  Niger watakamilisha kuondoka kwao katikati ya  Septemba

Wanajeshi wa Niger wakihudhuria ufunguzi wa mazoezi ya kila mwaka ya kukabiliana na ugaidi huko Niamey, Niger Aprili 11, 2018.
Wanajeshi wa Niger wakihudhuria ufunguzi wa mazoezi ya kila mwaka ya kukabiliana na ugaidi huko Niamey, Niger Aprili 11, 2018.

Wanajeshi wa Marekani walioamriwa kuondoka  Niger na utawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi watakamilisha kuondoka kwao katikati ya  Septemba, maafisa wa Pentagon na Niger walisema Jumapili.

Muda huo ulikuwa matokeo ya mazungumzo ya siku nne kati ya maafisa wa ulinzi wa nchi katika mji mkuu wa Niamey, kulingana na taarifa ya pamoja.

Uamuzi wa Niger kuwatimua wanajeshi wa Marekani ulikuwa pigo kwa operesheni za kijeshi za Marekani katika Sahel, eneo kubwa kusini mwa jangwa la Sahara ambako makundi yenye uhusiano na al-Qaida na kundi la Islamic State yanaendesha shughuli zake.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Niger wamefikia makubaliano ya kujiondoa ili kutekeleza uondoaji wa majeshi ya Marekani, ambao tayari umeanza.

Wajumbe kutoka pande zote mbili walithibitisha hakikisho la ulinzi na usalama kwa vikosi vya Marekani wakati wa kujiondoa

Forum

XS
SM
MD
LG