Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:23

Wanajeshi wa Kenya Washutumiwa Kufanya Biashara za Magendo


Picha ya Maktaba: Wanajeshi wa Kenya wakati wa tukio la Westgate
Picha ya Maktaba: Wanajeshi wa Kenya wakati wa tukio la Westgate

Ripoti mpya iliyochapisha na shirika la haki za waandishi wa habari “Journalist for Justice Rights,” imedai majeshi ya Kenya yaliyoko Somalia yanahusika na biashara za magendo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ripoti mpya iliyochapisha na shirika la haki za waandishi wa habari “Journalist for Justice Rights,” imedai majeshi ya Kenya yaliyoko Somalia yanahusika na biashara za magendo.

Magendo yanayohusishwa kufanywa na majeshi ya Kenya ni uuzaji wa sukari na makaa katika bandari ya Kismayu yenye thamani ya dollar millioni 400.

Kufuatia taarifa hizo, msemaji wa majeshi ya Kenya mjini Nairobi, Kanali David Obonyo, amekanusha vikali madai hayo.

Imedaiwa biashara hiyo inafanyika kwa ushirikiano na wakuu wa kijeshi mjini Nairobi kinyume na shabaha na malengo yaliyochangia kupelekwa kwa majeshi hayo nchini Somalia mwaka wa 2011.

Shirika hilo pia linadai wanajeshi wa Kenya wamehusika na ukiukaji wa haki za binadamu hususan ubakaji, mateso na kutekwa nyara kwa watu kutoka maeneo tofauti ya Somalia.

Taarifa imeongeza kwamba pia wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kufanya mashambulizi ya ndege ya mara kwa mara hasa maeneo yenye idadi kubwa ya raia ndani ya Somalia.

Na ingawa msemaji wa majeshi ya Kenya, Kanali Obonyo amekanusha vikali madai hayo, ripoti hiyo inadai imefanikiwa kupata habari hizo baada ya uchunguzi na utafiti mkubwa nchini Somalia na Kenya.

Pia maafisa wa shirika hilo wamedai kuwahoji wafanyabiashara wa sukari, madreva, maafisa wa serikali, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa pamoja na taarifa za kijasusi za mataifa ya magharibi nchini Somalia.

Pamoja na yote hayo Kanali Obonyo amesisitiza kwamba tuhuma hizo hazina msingi wowote na zipuuzwe.

Vile vile kumekuwa na tuhuma za wanajeshi hao kushirikiana na makundi ya Al Shabaab yanayohusika na biashara hizo haramu.

Tangu Kenya ipeleke wanajeshi wake Somalia baada ya misururu ya kutekwa nyara watalii na wafanyakazi wa mashirika ya kujitolea nchini Kenya, wanamgambo wa Al Shabaab wamefanikiwa kuishambulia Kenya.

Mashambulizi hayo yaliyoleta maafa makubwa ni ya Westgate na Chuo Kikuu cha Garissa.

XS
SM
MD
LG