Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 22:14

Wanajeshi sita wa Niger walinzi wa bomba la mafuta la Benin wauawa


Ramani inayoonyesha nchi za Niger, Nigeria, Chad, Cameroon na Benin
Ramani inayoonyesha nchi za Niger, Nigeria, Chad, Cameroon na Benin

Wanajeshi sita wa Niger waliokuwa wanalinda bomba la mafuta la nchi jirani ya Benin waliuawa katika shambulio la “majambazi wenye silaha” kusini mwa nchi, jeshi la Niger lilisema Jumapili.

“Wafanya doria wakujitolea waliokuwa wanalinda bomba hilo walishambuliwa na majambazi wenye silaha katika vitongoji vya kijiji cha Salkam, kwa bahati mbaya tunasikitishwa na vifo vya wenzetu sita,” jeshi lilisema katika taarifa.

Lilikuwa shambulio la kwanza kama hilo dhidi ya bomba la mafuta lenye urefu wa kilomita 2,000 ambalo linaounganisha kisima cha mafuta cha Agadem na bandari ya Benin ya Seme-Kpodii.

Jeshi la Niger limesema “limewalazimisha washambuliaji kukimbia” na kuua idadi isiyojulikana na kujeruhi washambuliaji hao.

Wanajeshi waliolengwa walikuwa katika operesheni dhidi ya ugaidi kwa miaka kadhaa na walikuwa wakifanya doria kusini mwa nchi karibu na mipaka na Nigeria na Benin.

Taarifa kuhusu shambulio hilo zimetokea siku mbili baada ya mvutano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Niger na Benin.

Forum

XS
SM
MD
LG