Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:12

Wanajeshi sita wa Mali wauawa katika shambulio la "magaidi wenye silaha", jeshi lasema


Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita

Wanajeshi sita wa Mali waliuawa katika shambulio lililofanywa na “makundi ya kigaidi yenye silaha” kaskazini mwa nchi, kulingana na ripoti ya jeshi.

Taarifa ya awali ya jeshi kuhusu tukio hilo ilisema mwanajeshi mmoja aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulio huko Ber siku ya Ijumaa.

Idadi ya vifo iliongezeka hadi sita, jeshi lilisema Jumamosi, likiongeza kuwa makundi ya magaidi wenye silaha waliacha nyuma miili 24”.

Waliacha pia bunduki aina ya AK-47 na pikipiki, jeshi limesema.

Limesema mapigano katika mkoa wa Timbuktu yalifanyika baada ya “jaribio la uvamizi na shambulizi la risasi la makundi ya kigaidi dhidi ya wanajeshi wa Mali”.

Wanajeshi wa Mali walitarajiwa kuweka kambi yao huko Ber kama sehemu ya makabidhiano, wakati tume ya Umoja wa mataifa nchini Mali inayojulikana kama MINUSMA, ikijiandaa kuondoka nchini humo, jeshi limesema.

Utawala wa kijeshi nchini humo uliopo madarakani tangu mwaka 2020, ulilishinikiza Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Juni kuondoa kikosi cha MINUSMA ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG