Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:12

Wanajeshi 6 wauwawa na wengine 25 wajeruhiwa nchini Mali


Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na askari kutoka kikosi kipya cha Takuba karibu na mpaka wa Niger huko Dansongo.
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria na askari kutoka kikosi kipya cha Takuba karibu na mpaka wa Niger huko Dansongo.

Wanamgambo wa Kiislamu waliwaua wanajeshi 15 na raia watatu wakati wa mashambulizi mawili tofauti kusini magharibi mwa Mali siku ya Jumatano, jeshi lilisema katika taarifa.

Wanajeshi sita walikufa na wengine 25 walijeruhiwa wakati wanamgambo walipovamia kambi ya kijeshi huko Sonkolo, eneo la mashambani kusini-kati mwa mkoa wa Segou, zaidi ya kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu Bamako.

Wanajeshi tisa na raia watatu waliuawa wakati wa shambulio la mapema asubuhi kwenye kambi tofauti katika mji wa kusini magharibi wa Kalumba, jeshi lilisema.

Kambi nyingine ya kijeshi katika mji wa kati wa Mopti pia ilishambuliwa wakati wa usiku, lakini washambuliaji walirudishwa nyuma bila majeruhi.

Mashambulizi yote hatimaye yalizuiliwa na wanajeshi waliwaua wanamgambo 48 huko Sonkolo, taarifa hiyo iliongeza.

XS
SM
MD
LG