Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:29

Wanajeshi 51 zaidi wauwawa Burkina Faso


Takriban wanajeshi 51 wameuwawa katika shambulizi la kustukiza linaloshukiwa kufanywa na wanajihadi kaskazini mwa Burkina Faso, jeshi limesema Jumatatu, na kuongeza kuwa washambuliaji  160 walifariki dunia katika mashambulizi ya kujibu mapigano. 

Shambulizi la kustukiza lilifanyika Ijumaa katika jimbo la Oudalan karibu na mpaka wenye vurugu wa Mali na Burkina Faso.

Mpaka kufikia mwishoni mwa Jumatatu, miili mipya 43 ilipatikana, na kufanya idadi ya awali ya vifo vya wanajeshi kufikia 51, jeshi lilisema katika taarifa.

Idadi hiyo ya vifo iliongezwa kwenye takwimu ya awali ya vifo vya wanajeshi wanane iliyotolewa na jeshi Jumatatu asubuhi.

Jeshi liliongeza kusema kwamba operesheni zinaendelea kwa kuongezeka mashambulizi ya anga ambayo viliwezesha kudhibiti magaidi 100 na kuharibu zana zao.

Burkina Faso inapambana na wanamgambo wenye msimamo mkali walioenea kutoka nchi jirani ya Mali toka mwaka 2015.

Ghasia hizo zimesababisha vifo zaidi ya 10,000, kulingana na makadirio ya mashirika yasiyo ya kiserekali na kusababisha watu milioni mbili kuyahama makazi yao.

Hasira ndani ya jeshi za kushindwa kukomesha umwagaji damu zimesababisha mapinduzi mawili mwaka jana.

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, jeshi lilitoa wito kwa watu wa Burkina Faso, kuungana na vikosi vya jeshi la ulinzi na usalama katika nyakati hizi ngumu.

Ombi hilo limekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Burkina Apollinaire Kyelem de Tembela kutangaza Urusi kuwa chaguo "la busara" la mshirika mpya katika vita dhidi ya jihadi.

XS
SM
MD
LG