Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:10

Wanajeshi 46 wa Ivory Coast wafikishwa mahakamani Mali


Wanajeshi 46 wa Ivory Coast ambao kuzuiliwa kwao na Mali kulizua mzozo wa kidiplomasia walifikishwa katika mahakama ya rufaa mjini Bamako, Alhamisi, kwa mujibu wa ripota wa AFP.

Kuonekana kwao kulikuja katika kipindi cha mwisho cha Januari 1 kilichowekwa na viongozi wa Afrika Magharibi, kwa Mali, kuwaachilia wanajeshi au kuwekewa vikwazo.

Wanajeshi 49 kutoka Ivory Coast walizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Bamako Julai 10.

Watatu, ambao wote ni wanawake, waliachiliwa.

Ivory Coast na Umoja wa Mataifa wanasema wanajeshi hao walisafirishwa kwa ndege ili kutoa usalama wa kawaida kwa kikosi cha Ujerumani cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, Mali.

Wajumbe wa Ivory Coast walikwenda Mali wiki iliyopita kwa mazungumzo juu ya mzozo huo, na wizara ya ulinzi ya Ivory Coast ilisema uko njiani kutatuliwa.

XS
SM
MD
LG