Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:05

Wanajeshi 19 waliotekwa nyara na waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati waachiliwa huru


Ramani ya Jamhuri ya Afrika ya kati
Ramani ya Jamhuri ya Afrika ya kati

Wanajeshi 19 waliotekwa nyara na waasi mwezi Februari kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati wameachiliwa huru, Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu (ICRC)limesema Jumanne.

Kati ya wanajeshi 20 waliotekwa nyara wakati wa shambulizi katika mkoa wa Vakaga tarehe 14 Februari, 19 waliachiliwa huru na walitarajiwa kuwasili katika mji wa Birao, na watabaki huko hadi maandalizi ya kuwarejesha mji mkuu Bangui yatapokuwa yamekamilika, naibu kiongozi wa tume ya ICRC Yves Van Loo ameiambia AFP.

Amesema wanajeshi hao 19 walionekana wana afya nzuri na waliweza kusafiri bila matatizo.

Van Loo amesema mwanajeshi wa 20 anapatiwa matibabu kwa majeraha na atapelekwa baadaye kwenye eneo tofauti.

Wanajeshi hao walitekwa nyara na kundi la waasi liitwalo Coalition of Patriots for Change (CPC) baada ya mapigano katika kijiji cha Sikikede, na serikali ilikiri kuwa ilipoteza wanajeshi wengi katika mapigano hayo.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ni moja ya mataifa maskini na yanayokumbwa na mzozo duniani, licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini.

XS
SM
MD
LG