Kambi ya kijeshi katika mji wa Tin-Akoff katika mkoa wa Oudalan karibu na mpaka na Mali ilishambuliwa vikali Jumatatu jioni, chanzo kimesema, kikitoa idadi ya 15 waliouawa huku wengine wakitoweka.
Jeshi la nchi kavu lilifanya shambulizi la kujibu kwa ushirikiano na jeshi la anga, na kuua magaidi kadhaa, chanzo hicho kimeongeza.
Chanzo cha pili cha vikosi vya usalama kimethibitisha shambulio hilo na kutoa idadi ya watu 19 waliouawa na wengine kadhaa kutoweka.
Shambulio hilo baya linajiri wakati taifa hilo la Sahel likiwa bado linatikiswa na shambulio baya la kushtukiza Ijumaa iliyopita karibu na mji wa Deou, pia katika mkoa wa Oudalan.
Wanajeshi 51 walifariki na wanamgambo wa kiislamu 160 kuuawa katika shambulio hilo na baadaye, kulingana na takwim za jeshi.
Facebook Forum