Kundi linalofanya uangalizi wa haki za binadamu Syria na lenye makazi yake Uingereza limesema kwamba kundi hilo lilifyatua makombora na roketi katika kituo cha jeshi la Syria, na kuua wanajeshi wanane karibu na Ruma katika jimbo la Idlib.
Kundi la HTS linaongozwa na wanachama wa zamani wa kundi la Syria lenye uhusiano na Al-Qaida.
Chombo cha habari cha serekali ya Syria hakikutoa taarifa za mapema kuhusiana na shambulizi hilo.
Takriban nusu ya eneo la jimbo la kaskazini mashariki mwa Idlib, na maeneo yanayo pakana na jimbo karibu la Aleppo, Hama na Latakia yamegubikwa na kundi la HTS na waasi wengine wanaokinzana.
Facebook Forum