Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:30

Wanajeshi 11 wauwawa Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria kwenye picha ya awali.
Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria kwenye picha ya awali.

Serikali ya Burkina Faso imesema kwamba wanajeshi 11 wameuwawa na wengine karibu darzeni mbili kujeruhiwa baada ya magaidi wenye itikadi kali kushambulia kambi ya kijeshi mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku baadhi ya washambuliaji wakiuwawa kupitia mashambulizi ya anga walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka mji wa Madjoari, katika jimbo la Kompienga, kulingana na taarifa ya jeshi.

Kwa miaka sita sasa, taifa hilo limekumbwa na ghasia zinazohusishwa na kundi la kigaidi la al Qaida pamoja na Islamic State, yakishukiwa kuua maelfu ya watu pamoja na kusababisha mamilioni kutoroka makwao.

Kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi ya serikali na kumuondoa rais alieyechaguliwa kidemokrasia hapo Januari liliahidi kurejesha hali ya utulivu, lakini badala yake mashambulizi yameongezeka nchini humo.

Ndani ya kipindi cha saa 72 wiki iliopita, karibu watu 60 waliuwawa wakati wa mashambulizi dhidi ya vijiji vinne kote nchini kulingana na ripoti ya ndani ya kiusalama.

XS
SM
MD
LG