Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:18

Wanainchi wa Senegal wapiga kura kuwachagua wabunge.


Watu wapiga foleni nje ya kituo cha kupigia kura katika kitongoji chenye wakazi wengi cha Ngor mjini Dakar, Julai 31, 2022. Picha ya AFP
Watu wapiga foleni nje ya kituo cha kupigia kura katika kitongoji chenye wakazi wengi cha Ngor mjini Dakar, Julai 31, 2022. Picha ya AFP

Wananchi wa Senegal Jumapili wamepiga kura katika uchaguzi wa bunge ambao upinzani una matumaini utalazimisha ushirika na Rais Macky Sall kuunda serikali na kuzuia nia yake ya kuwania muhula wa tatu.

Sall mwenye umri wa miaka 60, ambaye alichaguliwa mwaka 2012 kwa muhula wa miaka 7 na kuchaguliwa tena mwaka 2019 kwa muhula wa miaka mingine mitano, ameshtumiwa kwa kutaka kuvunja sheria kuhusu kikomo cha mihula miwili na kugombea tena mwaka 2024.

Bado hajasema wazi msimamo wake juu ya suala hilo, lakini kushindwa kwa wafuasi wake katika uchaguzi wa Jumapili kunaweza kuvuruga mipango yake.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi majira ya huko na vikaanza kufungwa saa kumi alasiri kwa duru moja ya upigaji kura ambapo raia milioni 7 wa Senegal walikuwa wanatarajiwa kupiga kura.

Matokeo ya kura yanatarajiwa kabla ya Ijumaa.

Kufikia mchana, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa asilimia 22, chanzo kilicho karibu na wizara ya mambo ya ndani kinachohusika na uchaguzi kimeiambia AFP.

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura katika vituo kadhaa vya kupigia kura ilionekana kuwa ndogo, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa AFP na wafuatiliaji.

XS
SM
MD
LG