Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:07

Wanaharakati washikilia ushahidi wa Nemtsov


Marehemu Boris Nemtsov, ambaye aliuwawa nchini Russia.
Marehemu Boris Nemtsov, ambaye aliuwawa nchini Russia.

Wanaharakati wa upinzani wa Russia, wanasema watachapisha hati zilizokusanywa na kiongozi wa upizani Boris Nemtsov, kabla ya kifo chake Febuari 27.

Hati hizo zinazotarajiwa kuonesha ushiriki wa kijeshi wa moja kwa moja wa Russia, katika vita ya Ukraine.

Mwanaharakati Ilya Yashin, mshirika wa karibu wa Nemtsov, alisema ushahidi huo ulikusanywa na mwanaharakati aliye uwawa Boris Nemtsov.

Unajumuisha taarifa zilizokusanywa kutoka kwa wazazi wa wanajeshi wa Russia, waliouwawa wakati wanapigana katika ardhi ya Ukraine.

Ameliambia gazeti la Uingereza The Times kwamba ushahidi ulikuwa umehifadhiwa vizuri na haujapotea wakati polisi waliposhikilia kompyuta ya bwana Nemtsov, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa mauaji yake.

XS
SM
MD
LG