Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:21

Wanaharakati Kenya wapinga marekebisho ya sheria ya misitu


Kenyan members of parliament maintain social distance amid the COVID-19 pandemic inside the Parliament buildings in Nairobi, June 10, 2021.
Kenyan members of parliament maintain social distance amid the COVID-19 pandemic inside the Parliament buildings in Nairobi, June 10, 2021.

Misitu kuzunguka mji mkuu wa Kenya, Nairobi, inayoendelea kukua kwa kasi imeibua mjadala kuhusu Marekebisho ya sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu ambayo sasa inajadiliwa na kamati ya bunge la nchi hiyo.

Wanamazingira wanasema marekebisho hayo huenda yakadhoofisha uwezo wa Huduma ya Misitu ya Kenya kupinga mabadiliko ya mipaka yaliyopendekezwa na kuhatarisha viumbe adimu au maeneo ya vyanzo vya maji.

Wanaounga mkono marekebisho hayo wanasema kubadili sheria kunawalinda watu ambao tayari wamekaa kwenye ardhi ya misitu inayozozaniwa.

Kenya ilipoteza takriban nusu ya misitu yake kati ya mwaka wa 1980 na 2000, kwa mujibu wa ripoti ya benki ya Maendeleo ya Afrika.

Kadhalika nchi hiyo ilipoteza asilimia 11 katika miongo miwili iliyofuata kwa mujibu wa ripoti ya Global Forest Watch.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG