Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 11:57

Wanaharakati wapinga uteuzi wa baraza la mawaziri Kenya


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi akiandamana na waziri wa mambo ya ndani, Fred Matiang'i.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi akiandamana na waziri wa mambo ya ndani, Fred Matiang'i.

Kundi la wanaharakati nchini Kenya Alhamisi liliwasilisha kesi mahakamani mjini Nairobi, kwa tuhuma kwamba baraza la mawaziri katika serikali ya Uhuru Kenyatta liliundwa kinyume cha katiba.

Wanaharakati hao wanataka baraza hilo livunjwe kwa sababu, wanasema, halikufuata maelekezo ya katiba ya nchi hiyo kwamba angalau theluthi moja wawe wanawake.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, waliowasilisha hoja hiyo ni Marilyn Muthoni Kamuru, Daisy Doreen Jerop Amdany na kituo cha haki, elimu na uhamasisho (CREAW).

Kesi hiyo pia inawajumuisha mwanasheria mkuu wa Kenya, katibu wa baraza la Mawaziri na bunge la nchi hiyo.

Kadhalika wanataka mahakama hiyo kuamuru kuwa hatua ya bunge la taifa ya kuidhinisha uteuzi wa mawaziri hao, haikuwa halali.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, uteuzi katika utumishi wa umma unafaa kutilia maanani kipengele kuhusu usawa wa jinsia, ambapo si halali kwa raia wa jinsia moja kuchukua Zaidi ya theluthi mbili ya nafasi za ajira.

XS
SM
MD
LG