Watu hao walikamatwa Jumatano wakati Zimbabwe inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa jumuia ya maendeleo ya ma dola ya kusini mwa Afrika (SADC) tarehe 17 Agosti na mkutano wa mwanzo kuhusu biashara na maendeleo ukiwa unafanyika.
Wanne kati ya wanaharakati hao waliondolewa ndani ya ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Harare siku ya Jumatano, chama cha mawakili wa Zimbabwe kilisema.
Wengine 14 walikamatwa katika mji mdogo wa kaskazini magharibi wa Kariba, chama hicho cha mawakili kilisema kwenye mtandao wa X.
Walishtakiwa Alhamisi chini ya sheria za kuvuruga usalama wa umma baada ya kushiriki katika maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani, Jameson Timba ambaye yuko kizuizini tangu mwezi Juni.
Forum