Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:54

Wanahabari 7 wakamatwa na polisi wa Somaliland.


Ramani ya Somaliland.
Ramani ya Somaliland.

Polisi katika jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland Jumatano wamewakamata waandishi wa habari saba, akiwemo mwandishi wa Sauti ya Amerika, walipokuwa wakiripoti kuhusu mzozo wa magereza katika mji mkuu wa jimbo hilo, Hargeisa.

Mwanahabari wa VOA Sagal Mustafe Hassan aliachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa muda mfupi, lakini wanahabari wengine waliobaki bado wanazuiliwa katika kituo kikuu cha polisi cha Hargeisa.

Miongoni mwa wanahabari waliokamatwa ni mwandishi wa BBC Hassan Gallaydh, mwandishi wa televisheni jimboni humo MM TV Mohamed Ilig na Ahmed Mohamud Yusuf wa kituo cha televisheni Saab TV.

Maafisa hawakusema kwa nini wanahabari hao walikamatwa, lakini wanahabari wenzao na ndugu wa wanahabari hao wameiambia VOA kwamba baadhi yao walikuwa wanatangaza moja kwa moja wakati wa kukamatwa kwao nje ya gereza, ambapo wafungwa wapatao 150, wafungwa wa uhalifu na ugaidi wanashikiliwa.

XS
SM
MD
LG