Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 12:08

Wanafunzi wa Sudan Kusini waandamana Uganda


Sudan na Sudan ya kusini zinazozana kuhusu umiliki wa eneo na Heglig au Panthou lililoko kwenye mpaka wa nchi hizi mbili.

Muungano wa wanafunzi kutoka Sudan kusini wanaosomea nchini Uganda wanautaka umoja wa Afrika kumteua kiongozi mwingine kuwa mpatanishi kati ya Sudan na Sudan Kusini na kumwondoa mpatanishi wa sasa Thambo Mbeki ambaye wamemuita "msaliti."

Wanafunzi waliyasema haya hii leo walipofanya maandamano ya amani mjini Kampala kupinga kushambuliwa kwa Sudan Kusini na Sudan.

Sudan na Sudan ya kusini zinazozana kuhusu umiliki wa eneo na Heglig au Panthou lililoko kwenye mpaka wa nchi hizi mbili.

Walijipanga na kuimba nyimbo katika maandanao kwa lengo la kufikisha ujumbe wao.

Wanafunzi waliondamana wanasema ikiwa serikali ya rais wa Sudan Omar el Bashir haitakubali kuzungumza na serikali ya Sudan Kusini basi hawatakuwa na budi kuipigania nchi yao.

Wanasema ujumbe kwa serikali ya Khartoum, ni kwamba watu wa Sudan kusini wako zaidi ya milioni kumi na tano, wameiomba serikali ya sudan kusini kuwahamasisha zaidi ya vijana milioni moja wajitolee wapate mafunzo ya kijeshi ili waweze kulinda nchi yao.

Raia wa Sudan kusini wanasema wamechoka kuchokozwa na Sudan. Waliyarejelea matamshi ya Rais Bashir siku chache zilizopita aliposema kuwa lugha anayoielewa ni ya bunduki na risasi. Wanasema matamshi kama haya ni ya uchokozi na hawataketi tu na kuiangalia Sudan ikiwachokoza.

Kwingineko, wanafunzi wameutolea mwito umoja wa Afrika kumteua kiongozi mwingine ambaye anaweza kuketi chini na Sudan zote mbili na kuzisaidia nchi hizi mbili kuelewana bila kuegemea upande mmoja.

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thambo Mbeki ambaye alipewa jukumu la kuzipatanisha Sudan na Sudan kusini na umoja wa Afrika analaumiwa kwa kuisaliti Sudan ya kusini.

XS
SM
MD
LG