Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 06:48

Wanafunzi wa Nigeria waitisha kurejea kazini kwa wahadhiri


Wafanyakazi wa Nigeria waandamana kuunga mkono mgomo wa wahadhiri
Wafanyakazi wa Nigeria waandamana kuunga mkono mgomo wa wahadhiri

Wanafunzi wa Nigeria Jumatatu wameshiriki kwenye maandamano ya kulalamikia mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya serikali, ambao umeathiri masomo ya takriban wanafunzi  milioni 2 na nusu nchini humo.

Wakati wakikaidi amri ya maafisa wa usalama kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Lagos,mamia ya wanafunzi walifunga barabara kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muhammed, suala lililotatiza baadhi ya safari za ndege.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, wanafunzi hao walibeba mabango wakiomba serikali kushugulikia wahadhiri hao ambao wamekuwa kwenye maandamano tangu Februari. Wakati maandamano hayo yakiendelea, mahakama moja nchini humo ilikuwa ikisikiliza kesi iliyowasilishwa na serikali, ya kuwalazimisha wahadhiri kurejea kazini.

Uamuzi wa kesi hiyo unatarajiwa kutolewa Jumatano. Migomo ya aina hiyo ni jambo la kawaida nchini Nigeria ambako kuna zaidi ya vyuo vikuu 100 vya serikali, na zaidi ya wanafunzi milioni 2.5.

XS
SM
MD
LG