Wiki iliyopita, wanafunzi wa kike 105 katika vyuo vikuu vya Afghanistan, wote wanawake kutoka jimbo la magharibi la Pakistan, Khyber-Pakhtunkhwa, linalo pakana na Afghanistan, walifanya maandamano katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakiomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa.
Waandamanaji Jumanne walitoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia, na kuiomba serekali ya Pakistan kutoa ufadhili maalumu kwa wanafunzi walio katika vyuo vya umma vya udaktari.
Hakuna serekali yoyote ambayo imeutambua utawala wa Taliban, hasa kutokana na wasiwasi pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu na namna wanawake wanavyo tendewa nchini Afghanistan.