Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 10:09

Abiria 32 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Tanzania


Watu 32 wakiwemo wanafunzi 29 wa shule ya msingi ya Lucky Vincent ya Kwa-Mrombo, Arusha,Tanzania, wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani mapema asubuhi Jumamosi.

Ajali ya basi la wanafunzi wa Arusha
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:08 0:00

Basi hilo lilikuwa limebeba waalimu 3 na dereva, msaidizi wake na wanafunzi 27. Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la shule kutumbukia katika korongo refu la mto Marera wilayani Karatu.

Vyanzo vya habari Tanzania vinaeleza kuwa mpaka sasa polisi wanaendelea na juhudi za kuondoa miili ya marehemu hao.

Taarifa za awali zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo, zikieleza kuwa basi dogo lilikuwa limebeba abiria 40, wengi wao wanafunzi na baadhi ya walimu.

Wanafunzi wa shule ya Lack Vincent muda mfupi kabla ya kusafiri na kupatwa na ajali ya basi
Wanafunzi wa shule ya Lack Vincent muda mfupi kabla ya kusafiri na kupatwa na ajali ya basi

Basi hilo liliondoka jijini Arusha saa moja asubuhi Jumamosi likielekea mji wa Karatu, ambako wanafunzi walikuwa washiriki katika mitihani ya majaribio pamoja na wanafunzi wenzao wa shule ya Wilaya ya Karatu

Baada ya mitihani hiyo, wanafunzi walikuwa wamepanga kutembelea mbuga ya Ngorongoro.

Wakati basi hilo lilipopita mji wa Rhotia Hill, likiwa katika kasi likishuka mlima kuja katika makutano ya barabara ya Kwa-Karani,' walioshuhudia ajali hiyo waliona basi likipaa hewani na kutumbukia katika korongo refu pembeni ya Mto Marera wilayani Karatu.

Miili ya wanafunzi walofariki kwenye ajali karibu na Arusha, Tanzania.
Miili ya wanafunzi walofariki kwenye ajali karibu na Arusha, Tanzania.

Rais John Magufuli ametoa taarifa kueleza masikitiko yake na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa, akisema ajali hiyo imezima ndoto ya watoto walokua wakijianda kulitumikia taifa lao.

XS
SM
MD
LG