Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:18

Wanafunzi Marekani wanatoa wito usitishaji ghasia za bunduki


Mwanasheria mkuu wa Florida, Pam Bondi katika mjadala wa usalama mashuleni

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas iliyopo Parkland walisafiri hadi kwenye bunge la jimbo la Florida nchini Marekani na kuwataka wabunge kupiga marufuku bunduki kubwa za hatari kama iliyotumiwa na kijana aliyesababisha vifo na madhara mengine katika shule yao.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Utawala wa Trump unajaribu kuweka kanuni kali zinazohusiana na ununuaji wa bunduki ambapo Rais Donald Trump amependekeza rasmi marufuku ya vifaa ambavyo vinageuza bunduki kuwa silaha ya hatari zaidi.

White House pia inaeleza kwamba wako tayari kuzungumzia kuweka vikwazo vya umri ambavyo mtu anaweza kununua bunduki za rashasha. Utawala ulieleza kwamba unaunga mkono uchunguzi wa kina kwa wale wanaotaka kununua bunduki. Rais alitangaza kutoka White House wakati wa sherehe za kutoa medali ya usalama wa juu zinazowapa heshima maafisa wa idara ya usalama.

Marufuku itajumuisha “BUMP STOCKS” kifaa kilichopo kwenye bunduki ambacho kinaruhusu kufyatua risasi nyingi kwa wakati mmoja ambacho kilitumika katika tukio la ufyatuaji risasi huko Las Vegas, Oktoba mwaka jana ambapo watu 58 waliuwawa na 851 walijeruhiwa.

White House inaaanda mjadala maalumu Jumatano ambao unawajumuisha wanafunzi, wazazi na waalimu ambao ni wahanga katika ufyatuaji risasi wa umma nchini Marekani. Pia washiriki wengine katika mjadala huo watakuwa wanafunzi kutoka shule ya sekondari huko Florida mahala ambako mwanafunzi Nikolas Cruz aliyefukuzwa shuleni hapo mwaka jana aliweza kuingia eneo la shule Jumatano iliyopita na kuuwa watu 17 katika muda wa dakika sita akitumia bunduki aina ya AR-15.

XS
SM
MD
LG