Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:31

Wanadiplomasia waongeza juhudi kumaliza ghasia Syria


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Saud Al-Faisal, kulia, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti Sheikh Sabah Khaled al-Hamad Al-Sabah kabla ya mkutano mjini Riyadh, Saudi Arabia,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Saud Al-Faisal, kulia, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti Sheikh Sabah Khaled al-Hamad Al-Sabah kabla ya mkutano mjini Riyadh, Saudi Arabia,

Mkutano wa "Marafiki wa Syria" Jumapili huko Istanbul unatazamiwa kuongeza shinikizo la kupata ufumbuzi wa mgogoro wa nchi hiyo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton anakutana na wanadiplomasia wa nchi za Ghuba huko Saudi Arabia kujadili namna ya kumaliza mgogoro ya kisiasa Syria ambao umefikia mwaka mzima sasa.

Mkutano huo ni matayarisho ya mkutano wa nchi 60 zinazojita "Marafiki wa Syria" utakaofanyika Istanbul, Uturuki Jumapili. Clinton pamoja na wanadiplomasia kutoka nchi nyingine zinazounga mkono makundi ya upinzani ya Syria wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo wa Istanbul.

Marekani ingali inapinga kuwapa silaha waasi wa Syria, hatua ambayo imependekezwa na baadhi ya nchi za Ghuba. Washington badala yake inajaribu kuleta ushirikiano wa makundi mbali mbali ya upinzani nchini humo, na kufikisha misaada ya kibinadamu ndani ya Syria.

Kabla ya mkutano wa Istanbul, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu alisema mpango wa amani uliowasilishwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu Kofi Annan ni kiwango cha mwisho kabisa ambacho Syria inatakiwa kukitekeleza bila "ucheleweshaji wowote."

XS
SM
MD
LG