Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:31

Uingereza kuwatimua wanadiplomasia 23


Polisi wa Uingereza wakilinda eneo ambalo jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal anaishi huko Salisbury, Uingereza, Jumanne Machi 13, 2018
Polisi wa Uingereza wakilinda eneo ambalo jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal anaishi huko Salisbury, Uingereza, Jumanne Machi 13, 2018

Uingereza imesema itawafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi baada ya Moscow kukataa kutoa maelezo vipi aina ya sumu iliyokuwa ikitumika wakati wa utawala wa Soviet ilivyotumika katika mji wa Salisbury- Uingereza kumshambulia jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake, Yulia.

Kulipiza kisasi kuliko tangazwa Jumatano na Waziri Mkuu Theresa May katika Bunge la Uingereza kunapelekea kuanza kwa vita ya kiuchumi dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na kikundi cha watu wachache wenye maslahi ya pamoja cha maafisa wa serikali ya Kremlin na wafanyabiashara matajiri wenye ushawishi wa kisiasa.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuia rasilmali zao ambazo wanazimiliki Uingereza pamoja na kunyimwa viza kwa watu binafsi wote waliotajwa katika sakata hilo.

Waziri Mkuu anawashinikiza washirika wa kimataifa kufuata hatua iliyochukuliwa na Uingereza na kuanza kuangaza mabilioni ya dola ambazo Kremlin imewekeza katika rasilimali zake ulimwenguni kote.

Lakini maafisa wamesema hata hizo hatua zilizochukuliwa na Uingereza peke yake zitasababisha machungu kwa Warusi ambao wanamafungamano na Kremlin, ambayo, chini ya mpango uliowekwa na Uingereza, rasilimali na mali zao zote zitachukuliwa, iwapo hawatoweza kuonyesha chanzo cha mali na rasilimali zao zimepatikana kwa njia halali.

Maafisa wa serikali ya Uingereza wanauwezo chini ya sheria ya fedha zinazotokana na uhalifu kuanza kuchukua hatua kukamata rasilimali za Urusi.

“Kwa jumla kile ambacho tumepanga kufanya kitakuwa na athari mbaya sana kwa Urusi,” afisa wa ngazi ya juu wa Uingereza ameiambia VOA.

​
XS
SM
MD
LG