Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 16:55

Wapiganaji saba wa Al-Shabab wauwawa Somalia


Wanamgambo wa Al Shabab

Maafisa wa Somalia wanasema kamanda wa Al- Shabab ni miongoni mwa waliouwawa kutokana na kombora lililofyetuliwa na ndege isiyotambulika.

Mashahidi wanasema shambulizi la anga limeuwa wanachama saba wa Al shabab kundi lenye uhusiano na Al Qaida kusini mwa Somalia.

Shambulizi hilo limetokea mapema leo katika eneo linalodhibitiwa na waasi linalojulikana kama kilomita 60, kusini mwa mji mkuu Mogadishu.

Maafisa wa Somalia wanasema kamanda wa Al- Shabab ni miongoni mwa waliouwawa wakati kombora liliporushwa kutoka kwenye ndege ambayo haikutambuliwa na kupiga kwenye gari .

Mwandishi wa habari wa idhaa ya kisomali ya Sauti ya Amerika anasema waliofariki ni wasomali watatu na raia wanne wa kigeni.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo. Vikosi vya usalama vya Marekani vimejulikana kufanya mashambulizi huko Somali hasa la hivi karibuni mwezi Januari ambako makomandoo wa jeshi la majini liliwaokoa wafanyakazi wawili wa msaad ambao walikuwa wanshikiliwa na maharamia.

XS
SM
MD
LG