Meli za mapumziko hivi sasa ziko huru kuomba uthibitisho wa chanjo ya virusi vya Corona kutoka kwa abiria wake katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Jaji mmoja wa serikali kuu ya Marekani alitoa amri ya awali kwa meli ya Norway ya Cruise Line hapo Jumapili kuiwezesha kuwauliza abiria wao hali zao juu ya uthibitisho wa chanjo ya virusi vya Corona.
Tunakaribisha uamuzi wa leo ambao unaturuhusu kusafiri kwa meli na wageni pamoja na wafanyakazi waliopatiwa chanjo kwa asilimia mia moja, jambo ambalo tunaamini ni njia salama nay a busara zaidi kuanza tena shughuli za kusafiri kutokana na janga hili la ulimwengu, Frank Del Rio, rais na mtendaji mkuu wa kampuni ya Norwegian Cruise Line Holdings alisema katika taarifa.
Amri hiyo inafuta agizo la gavana wa jimbo la Florida, Ron DeSantis aliyoisaini kuwa sheria mwanzoni mwa mwaka huu, ambayo ilizitoza faini biashara ambazo inataka uthibitisho wa chanjo ya virusi vya corona kutoka kwa wateja.