Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:43

Makampuni ya Canada yafurahia wazo la Wamarekani kuhamia huko


Makampuni kadhaa ya Canada yanafurahia wazo linalojitokeza hapa Marekani kila wakati uchaguzi unapokaribia la wamarekani kuhamia nchini humo.

Baadhi ya wamarekani husema kuwa maisha yatakuwa magumu chini ya utwala wa kiongozi fulani na kwa hivyo kusema kuwa watahamia Canada hata ingawa takwimu zinaonesha kuwa hilo huwa halitokei.

Wengi wamekuwa wakiingia kwenye mtandao wa Google wakiuliza jinsi ya kuhamia Canada hasa wakati huu ambapo uchaguzi za awali zinaendelea katika majimbo tofauti.

Hilo lilishuhudiwa tena jumanne usiku baada ya Donald Trump kushinda kwenye uchaguzi wa awali wa Indiana huku uwezekano wake wa kuwa mgombea wa urais kwa chama cha Republikan ukijitokeza.

XS
SM
MD
LG