Hayo ni kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa, akiongeza kwamba rais Joe Biden angali ana nafasi ya kutumia hifadhi ya ziada ya mafuta ya Marekani, ili kudhibiti bei za mafuta ambazo wenye magari wanalipia kwenye vituo vya kujazia.
Brian Deese ambaye ni mratibu wa baraza la kitaifa la uchumi wakati akizungumza na televisheni ya NBC kipindi cha Meet the Press amesema kwamba bila shaka kuna mfumuko wa bei unaoathiri mifuko pamoja na muonekano wa wamarekani.
Bei za bidhaa hapa Marekani zilipanda kwa asilimia 6.2 mwezi uliopita, likiwa ongezeko kubwa zaidi tangu mwaka 1990, kulingana na ripoti ya wizara ya kazi ya wiki iliyopita.
Ongezeko la bei za nishati na chakula limeathiri wanunuzi wengi wakati asilimia 70 ya mapato hapa Marekani ikisemekana kuenda kwenye bidhaa hizo muhimu. Deese wakati wa ripoti hiyo hakutoa suluhisho lolote la hivi karibuni. Lakini amesema kwamba wadadisi wanatarajia kwamba viwango vya mfumuko vitashuka kufikia mwaka ujao.